“Kwa sasa, hakuna kazi ya wavulana wala wasichana, sote tunaweza”

Alice Nifasha ni mojawapo ya wasichana wanaofanya kazi ya kunyoa nywele za watu. Hapo zama za kale, Sanaa ya kunyoa nywele ilikuwa ikionekana kama kazi iliyotengewa wavulana tu. Tulipomkuta akiwa anafanya kazi, aliweza kutushuhudia namna alivyoanza Sanaa hiyo na faida aipatayo kutoka hapo. Alice Nifasha alitushuhudia tena changamoto tofautitofauti zilizomkumba wakati alipoanza kazi hiyo. Ni kawaida, mtu anapoanza kufanya kinachomkereketa ili kujitunza kimaisha, lazima kuwe na vizuizi vya wanaotaka kumkata tamaa na kumrudisha nyuma. Ila suluhisho la yote, mara nyingi ni kutosikia watu kama hao ikiwa amejinusuru kupambania maendeleo yake…